kwamamaza 7

Sisi si watumwa wa majirani- Rais Kagame

0

Rais Kagame amewambia wananchi Wilayani Burera, Kaskazini nchini Rwanda kwamba Wanyarwanda siyo watumwa wa majirani wao.

Rais Kagame katika Ziara yake ya kazi, amesema kwamba miaka kadhaa kuna watu wanaolenga kuletea Rwanda changamoto na kuwataka wanachi kulinda nchi kama inavyostahili.

“ Sisi si watumwa wa majirani. Hatuko watu wa kuonewa. Lakini viongozi wasipofanya vizuri, inazua matatizo. Mengi mnayoyatafuta nje ya mipaka yangali hapa, mnayacha hapa. Viongozi wanakaa mjini na kudhani kuwa huo ni mwisho wa ulimwengu.” Rais Kagame amesema

Rais Kagame ameweka wazi kwamba aliwahi kuambiwa kuna watu wanaovuka mpaka ili kununua mkate na kuongeza “ Watoto wanaokwenda nchini Uganda kutahiriwa kwa kutumia pete wakati ambapo huduma hii ilibuniwa na inatolewa nchini Rwanda.”

Mheshimiwa Kagame amesema hayo yote ni matokeo ya viongozi ambao hawatimizi wajibu wao kama ilivyo.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.