kwamamaza 7

Serikali ya Rwanda yashtumiwa mauaji dhidi ya raia- ripoti ya HRW.

0

Baada ya ripoti ya awali ya Shirika la Kutetea Haki za Kibinadamu (HRW) kuzinduliwa ikieleza kuwa wakaazi wa Rwanda wamejawa na hofu ya kutukia kwa ghasia  nyakati hizi za uchaguzi kumefuatia ripoti nyingine ikilishtumu jeshi la usalama la Rwanda mauaji dhidi ya raia.

Katika ripoti hii iliyozinduliwa Alhamisi tarehe 13 Julai, Rwanda inashtumiwa kuwaua raia wa Rwanda kupitia majeshi ya Usalama ambao wanashirikiana na viongozi wa kawaida. Katika ripoti hii inasemekana majeshi ya polisi na askari jeshi limekuwa likiwakamata raia kwa makosa madogo kama uizi, na kuwaua bila kuwepo kesi mahakamani.

Ripoti hii inasema zaidi kwamba takriban ya watu 37 wameuawa na majeshi ya usalama kwa makosa madogo kama uizi wa kawaida na hasahasa wa mifugo na ripoti hii inaendelea kusema kwamba kuna watu wengine wane ambao hadi sasa hakuna anayejua walipo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hata hivyo waziri wa Sheria Johnston Busingye amelaani vikali ripoti hii kwa kusema ni madai yasiyo na msingi yenye makusudi ya kujitangaza tu.

Waziri huu amesema kupitia ukurasa wa twitter kwamba shirika hili lina lengo la kuifanya kazi yake kutiwa maanani hadi kutoa ripoti potofu dhidi ya serikali ya Rwanda.

Ameagiza kwamba ni wakati wa Shirika lile la kutetea haki za kibinadamu lianze ufanyajikazi kwa kitalaam .

“Huu ni wakati wa mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kuwa wenye uzoefu wa kazi kwa kuonyesha utalaam wa kazi yao kusiko biashara ya haki za kibinamu”.

 Ameongeza ya kwamba Rwanda itaendelea kufanya mambo yake kwa namna yake kwa kuwa inawafaa Wanyarwanda.

Hii si mara ya Kwanza kwa serikali ya Rwanda kuzilaani ripoti za Shirika la Kutetea Haki za Kibinadamu la HRW kwa kuwa siku za hivi karibuni tu wizara ya sheria iliikana madai ya ripoti ya shirika hili yaliyokuwa akisema kwamba raia wa nchi ya Rwanda wano hofu nzito kwamba kunaweza kukatukia ghasia.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.