HABARI MPYA

Serikali ya Rwanda yakana mashtaka ya shirika la kutetea haki za binadamu,HRW

Serikali ya Rwanda kupitia waziri wa haki,Johnston Busingye amekana mashtaka ya shilika la kutetea haki za binadamu,HRW, ya kuwatesa kimwili na kufunga jela kinyume watuhumiwa wa ushirikiano na makundi ya wanamgambo kama vile FDLR na RNC.

Waziri Busingye kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mikononi,ametangazia VOA kwamba hawahojiani tena na shilika hili na kuwa yaliyomo katika ripoti hii ni uongo mtupu ambao shilika hili haliwezi kufafanua.

Hakuna ushirikiano kati yetu na shilika hili,haya ni mashtaka yasiyo kuwa na uthibitsho kulingana na sheria”ameleza Waziri Busingye.

Serikali imetangaza haya wakati ambapo ripoti hii yenye makaratasi 91 ya HRW, inasema kuwa watu 104 mwa walioulizwa katika utafiti wa huu walieleza kuteswa kimwili kama vile kupigwa nyaya za umeme,kumwagikiwa asidi kwenye mwili na mengine ili kukubali kwa nguvu kuwa na hatia.

Hawa walitangaza kuwa walifanyiwa haya walipofungiwa vituo vya wanajeshi kama vile Mukamira,Bigogwe,Mudende,Kami na kwenye makao makuu ya wizara ya Kijeshi,Kimihurura.

Mala nyingi serikali ya Rwanda hukana ripoti za HRW kwa kueleza kuwa zinaegamia upande mmoja na kuwa zinadhamiria kupaka masizi serikali ya Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top