HABARI MPYA

Serikali ya Rwanda kusaidia wakazi kupambana na umasikini

Waziri mkuu,Dk. Edouard Ngirente ametangaza kuwa serikali inatarajia kusaidia wakazi kupambana vilivyo na hali ya umasikini hasa wale wadogo ambao wanaishi katika hali hii kwenye mamlaka ya miaka saba.

Waziri mkuu ametangaza haya akiwa kwenye mkutano kwa jina la ‘Umushyikirano’ unaotokea kwa mala ya 15.

Waziri mkuu Ngirente kwenye hotuba yake amesema kuwa kutatiliwa mkazo mambo ya maisha mazuri ya wakazi ili kila Mnyarwanda aweze kupata ujuzi na kuishji katika familia nzuri.

Pia waziri mkuu amesisitiza kuwa hili si ndoto na kuwa litawezekana kupitia bidii za Wanyarwanda hasa vijana kwa kutumia fursa watakayopatiwa.

Mbali na kupambana na ufukara,waziri mkuu amesema kuwa serikali italinda na kuboresha yaliyotimizwa miaka iliyopita kwenye mamlaka hii mpya ya miaka saba.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top