kwamamaza 7

Serikali ya Burundi yatuhumiwa kusaidia kambi za jeshi za RNC

0

Chombo  cha habari nchini Kenya The Standard kimeweka wazi serikali ya Burundi inasaidia kazi za kila siku za kambi za jeshi za chama cha upinzani kwa Rwanda, RNC cha Jen. Kayumba Nyamwasa.

Hizi taarifa zimeeleza serikali ya Burundi inasaidia kambi za RNC zilizo nchini DR Congo eneo la Minembwe, Kusini Kivu.

“ RNC ina kambi za jeshi nchini DR Congo zinazosaidiwa na serikali ya Burundi” The Standard imetangaza

Isisahaulike kwamba chombo kingine cha habari nchini Uganda kwa jina la Virunga Post kilitangaza kwamba  kuna kundi la vijana 43 ambao walikamatwa mwezi Disemba 2017 wakijaribu kuvuka mpaka kati ya Uganda na Tanzania ili kuenda nchini DR Congo kupitia Burundi.

Hiki chombo cha habari kilieleza Mkuu wa Jeshi la Burundi,  Jen. Prime Niyongabo anawasindikiza wanaosajiliwa na RNC  kuenda katika kambi za jeshi huko Minembwe.

Kwa upande mwingine, Msemaji wa RNC, Jean Paul Turayishimiye alitangazia Sauti ya Marekani kuwa haya madai ya kuwa kuna  wanajeshi wao nchini DR Congo ni uongo mtupu.

Kwa sasa serikali ya Burundi haijafunguka lolote kuhusu haya madai ya The Standard.

Fred  Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.