Serikali ya Burundi imepiga marufuku madai ya mmoja mwa viongozi wa wanamgambo kutoka Rwanda, Callixte Nsabimana maarufu kama Sankara aliyesema kwamba alisaidiwa na Meja. Bertin, kiongozi wa upelelezi wan je nchini Burundi.

Sankara, 37, aliyekuwa mahakamani baada ya kukamatwa, alisema kuwa alikutana na Meja Bertin na kumshauri namna ya kukutana na maafisa wa upelelezi nchini Uganda.

Hata hivyo, Kiongozi ambaye hakutaka jina lake litangazwe ameambia Chimpreports kuwa Burundi haina afisa kwa jina hilo.

“ Hatuna na hatukuwa na muntu ayitwaye Meja Bertin. Hajulikani huku,” amekanusha

Wanyarwanda wanaweza kukuambia huyo Bertini nani kwani sisi hatumujui.” Ameongeza

Pamoja na hayo, ripoti ya watalaam wa Umoja wa Mataifa mwaka 2018, ilionyesha kwamba Burundi inawaunga mkono wanaolenga kuvamia Rwanda. Burundi ililaani mashtaka hayo.

 

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.