HABARI MPYA

Rwanda:Wendesha mashtaka wa kikanda wahamasishwa kuwakamata watuhumiwa wa mauaji ya kimbali

Mwendesha mashtaka mkuu wa Rwanda,Jean Bosco Mutangana ameomba wendesha mashtaka wakuu wa nchi zikiwemo Kenya,Uganda,Sudani Kusini na Tanzania kutoa msaada wa kuwakamata watuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 wanaojificha nchini zao.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Rwanda,Jean Bosco Mutangana

Kwenye mkutano wao,mwendesha mashtaka Jean Bosco Mutangana amehamasisha wendesha mashtaka wenzake kujali hati za kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya kimbali zilizotolewa na Rwanda.

Pia Mutangana amendelea kusema kwamba hata kama ni vigumu kuwakakamata,haina budi kufanya juu chini wakamatwe na kuhukumiwa nchini hizo au watumwe nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa taarifa za The NewTimes,Jean Bosco Mutangana amesisitiza kwamba hili litazuia kutojali katika eneo la nchi hizi.

Baraza hili la wendesha mashtaka wa kikanda liliundwa mwaka 2010.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top