HABARI

Rwanda:Wathirika wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi wamtetea Dk.Kabirima

Wathiriwa 5 wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 wamemtetea Dk.Jean Damascene Kabirima anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbali wakisema kwamba shutuma ni uongo bali ni migogoro ya awali husika na mashamba.

Baadhi ya wanaomtetea kuna Jean Baptiste Kayiranga anayeishi mjini Kigali,Angelbert Nkusi,Vincent Nzirabatinyi,Francois Bihoyiki na Stefano Ndahunga wanaoishi alikozaliwa Dk.Kabirima, wilaya ya Nyaruguru.

Bw Kayiranga amesisitiza kwamba alimjua Kabirima alipokuwa mjini Kigali wakati wa mauaji ya kimbali,madai yanayosisitizwa na Angelibert Nkusi aliyekana madai ya wanawe wakiwemo Mukazera anayesema kwamba Kabirima alimbaka na ndugu ye Mazimpaka anayeleza kwamba Kabirima alishiriki katika kundi lililokuwa likiwinda Tutsi kijijini Bunge.

Mzazi huyu amethibitisha kuwa wanawe wanadanganya kwa kuwa yeye aliwapeleka nchini Burundi bila jeraha wala kupigwa fimbo.

Hawa wote wamesisitiza kwamba shutuma hizi ni kwa sababu ya migogoro husika na mashamba inayodumu kwa miaka 34

Dk.Jean Damascene Kabirima alikamatwa alipohudhuriya mkutano mijini Kigali mwaka 2011. Kesi hii itaendelea tarehe 10 Octoba mwaka 2017.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

@Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top