HABARI

Rwanda:Walimu hawakubaliani na namna inayotumiwa kuwatuza wenzao

Walimu wametangaza kwamba hawakubaliani na namna ambayo inatumiwa kupatia tuzo walimu waliofanya kazi yao vizuri.

Mmoja wao ametangazia VOA kuwa hakubaliani na  namna ambavyo zawadi hizi zikiwemo tarakirishi na ng’ombe zinatolewa kwa kuwa walimu wote hufanya kazi sawa na kuwa kazi hii ni bega kwa bega.

Sisi sote humaliza siku nzima tukiwa shuleni,sielewi namna ambavyo mwalimu mmojaanaweza kufanya kazi kuliko mwingine”ameleza.

Huyu amependekeza kutolinganisha mwalimu wa shule ya msingi na wale wa shule ya sekondari wakati wa  kutoa tuzo hizi.

Jambo hili lilifafanua mara nyingi na viongozi husika kuwa zawadi hizi ni kwa lengo la kuwapa motisha walimu waliofanya waziwazi kazi yao kwa bidii kuliko wengine.

Wizara ya elimu imehamasisha walimu kufanya kazi kama wazazi kuliko kuwa walimu ili kupiga shabaha la ubora wa elimu jambo ambalo walimu wanaona kuwa gumu mno kwa kuwa wanakumbwa na tatizo la mshahara mchache.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top