HABARI MPYA

Rwanda:Wahalifu wa makosa madogo kuadhibiwa kufanya kazi zenye manufaa kwa umma

Waziri wa kutetea katiba na sheria nyingine,Evode Uwizeyimana wakati wa kuweka hadharani kanuni mpya za adhabu ameleza kuwa wahalifu wa makosa madogo hawatafungwa jela ila watadhibiwa kufanya kazi zenye manufaa kwa umma.

Waziri Evode Uwizeyimana ameleza kuwa hili ni kugawanya idadi ya wafungwa na kiasi cha pesa kilichokuwa kikitolewa kuwasaidia wafungwa.

Waziri huyu amewakumbusha wafungwa kuomba madhabu ya kufanya kazi zenye manufaa kwa umma wakati wa kujadili kesi zao badala ya kufungwa gerezani.

Hili linahusiana na maombi ya mashirika mbalimbali ya haki za binadamu kuwa kunahitajika namna ya kuadhibu wahalifu wa makosa madogo badala ya kuwafungwa jela.

Kanuni mpya inaundwa na karasa 360 badala ya 766 za kanuni iliyokuwepo,kanuni hizi zitafanyiwa uchunguzi na wabunge kupitia tume ya siasa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top