kwamamaza 7

Rwanda:Radiyo iliyofungwa yashtaki Rwanda Media Commission(RMC)

0

Mwanasheria Me Rugaza David na Mkurugenzi Pastor  Grek Schoofe wa Radiyo iliyofungwa Amazing Grace  wamefika mahakamani wilayani Nyarugenge ili kushtaki RMC kuhusu kufunga hii Radiyo.

Huyu  mwanasheria ameeleza jaji kuwa  wameamua kushtaki RMC badala ya RURA iliyoamua kufunga Radiyo Amazing Grace  kwa kuwa kanuni za kazi ya Utangazaji zinaeleza makosa yote yanaadhibiwa na RMC.

Kwa mjibu wa taarifa za Flash TV,Me Rugaza ameeleza 14 Februari 2018 RMC iliandikia RURA  ikiomba kufunga hii Radiyo kulingana na mkataba wa ushirikiano uliotiliwa saini mwaka 2013.

Mwanasheria wa RMC, Me Francois Kayigire amesema wangelishtaki RURA kwani iliamua kufunga Radiyo Amazing Grace.

Huyu amesisitiza waliandikia RURA wakitoa  ombi tu na kuwa uamuzi wa RURA  ulikuwa  kinyume na ombi lao.

Mwanasheria wa Radiyo Amazing Grace,Greg Schoofe ametaka mahakama  kuhukumu RMC kutoa faini ya frw miliyoni 50.

Upande wa washtakiwa umeitaka mahakama  kuhukumu wanaoshtaka kulipa fedha za mwanasheria na faini frw miliyoni tano.

Radiyo Amazing Grace ilifungwa na RURA mwezi  Februari juu ya ujumbe ilioptisha uliodaiwa kupaka masizi wanawake.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song update

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.