HABARI MPYA

Prof.Silas Lwakabamba,asili yaTanzania ajiuzulu kuongoza chuo cha Kibungo,UNIK

Prof.Silas Lwakabamba aliyewahi kuwa waziri wa elimu pia na wa miundo mbinu amejiuzu kuongoza chuo cha Kibungo kwa jina la UNIK kwa sababu binafsi.

Prof.Silas Lwakabamba

Kupitia Radiyo Flash,asubuhi hii Lwakabamba ametangaza kwamba amejiuzulu kwa sababu ya ukosefu wa matokeo wakati wa miaka miwili anayotimiza akiongoza chuo cha UNIK.

Amendelea kwa kusema kuwa hakuweza kutimiza wajibu wake kama vile kuleta maendeleo ya shule,kuboresha elimu kwa sababu ya changamoto za viongozi wa chuo hiki.

Ameongeza kwamba alianzisha mikakati mbalimbali kama vile kuongoza idadi ya wanafunzi lakini viongozi wakuu hawakukubali wala kukana.

Prof.Silas Lwakabamba amekana kwamba kujiuzulu kwake kuna uhusiano na madai ya itikadi ya mauaji ya kimbali yaliyowahi kujitokeza kwa kuwa watu husika waliamua kuwa madai haya yalikuwa fununu.

Prof.Silas Lwakabamba ni Mnyarwanda menye asili  nchini Tanzania, aliongoza shule kuu la teknologia na usimamizi(KIST) na chuo kikuu cha Rwanda.

Prof.Silas Lwakabamba amejiuzulu baada ya taarifa zilizotangazwa kwamba alikuwa akipata mshahara usohusika na matokeo,kupendelea Mtanzania aliyekuwa  mshauri wake na itikadi ya mauaji ya kimbali.

Kupitia ujumbe mfupi kwa simu ya mikononi,ametangazia Bwiza.com kwamba haya yote ni uwongo mtupu.

Haya yote ni uwongo mtupu,hakuna ukweli ndani”amesema Prof.Silas Lwakabamba

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top