HABARI MPYA

Rwanda:Ofisi  kuu ya wafungwa na magereza yakana mashtaka ya wanasheria wa Dkt. Leon Mugesera

Ofisi kuu ya wafungwa na magereza(RCS)imekana shutuma za wanasheria wa Dkt.Leon Mugesera aliye gerezani kwamba anateswa.

Wansheria kutoka nchini Kanada wakiongozwa na David Pavot walishtaki kwenye mahakama ya Afrika ya haki za binadamu naza wakazi kuwa Dkt.Leon Mugesera angali katika hali mbaya gerezani na kuwa haki zake zinakiukiwa.

Baada ya haya,tarehe 28 Septemba 2017 mahakama iliamua kuwa serikali ya Rwanda haina budi kumpa Mugesera rukhusa ya kukutana na familia yake,wanasheria wake na kuacha kamwe kumtesa kimwili wala kibongo.

Kwa upande mwingine spika wa RCS, CIP Hillary Sengabo amekana madai haya na kueleza kwamba Dkt.Leon Mugesera anaishi katika hali sawa na ile ya wafungwa wenzake.

Mwanamke wake,Gemma Uwamariya na mwanawe Carmen Nono wametangaza kufurahia hukumu hii kulingana na taarifa za lapresse.ca

Rwanda ina siku 15 za kupiga rufaa ya uamuzi huu wa mahakama.

Dkt.Leon Mugesera alikamatwa mwaka 2012 nchini Canada na kutumwa nchini Rwanda alipohukumiwa   maisha jela kwa mchango wake mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top