HABARI

Rwanda:Mkutano wa baraza la mawaziri wathibitisha mipango ya miaka saba

Mkutano usio wa kawaida wa baraza la mawaziri jana ulithibitisha mipango mbalimbali ya serikali wakati wa miaka saba.

Baadhi ya mipango hii ambayo kwa mala nyingine ni fikra za chama tawala yaani RPF-Inkotanyi kuna kuunda kazi mpya, kutoa msaada kwa miradi ya teknolojia na ubunifu,maendeleo ya miji,vijiji na majengo na mengine husika na makazi.

Pamoja na hayo, seriakli itatilia mkazo mambo ya miundo mbinu hasa barabara zinazoounga wilaya mbalimbali zenye ulefu wa km 800 na kukarabati nyingine zenye ulefu wa km 3,000 na barabara mpya zenye ulefu wa km 350.

Pia,serikali itaungana mkono na wafanyabiashara binafsi kuhusu uanzishaji wa viwanda mpya kama vile kiwanda cha dawa,chandarua,nguo,mbolea na mengine.

Tena kuna mpango wa kujenga bandari kavu na kuongeza sitaha inayomwagiwa maji kwenye kiwango cha 12% kila mwaka ili kupambana na machafuko ya mazingira.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top