HABARI MPYA

Rwanda:Malalamiko ya wanafunzi na wazazi wakati kunasubiriwa uthibitisho wa mabadiliko ya chuo kikuu cha nchi

Wanafunzi wa chuo kikuu(UR) na wazazi wao wameweka wazi kulalamikia mabadiliko ghafla kwenye chuo kikuu yakiwemo kuhamishia na kufuta kampasi zake.

Kiongozi makamu wa UR kwa wajibu wa maendeleo,Dkt Charles Muligande

Baadhi ya wanafunzi wametangaza kwamba hawakujua mabadiliko haya ili kujitayarisha,mmoja wao Patrick Mutabazi,mwanafunzi wa teknolojia,II amesema kwamba wangelipatiwa muda wa kutosha ili kuwa tayari badala ya kuwajulisha wiki tatu kabla ya kwanza mwaka wa masomo.

Hatukupatiwa muda wa kujitayarisha,ni vigumu kuhamia Butare kuenda Kigali”ametangazia The New Times.

Kwa upande wa wazazi wametangaza kuwa mabadiliko ghafla haya yanahitaji fedha nyingi kuliko kawaida,mmoja wao Edith Nyirabera ambaye binti ye atahamia Kigali amesema kuwa hii itakuwa hali ngumu mno kwake.

Nilikuwa nikilipa frw 6,500 za makazi kila mwezi,lakini nilipokwenda Kigali kutafuta makazi ya mwanangu ilinibidi kulipa frw30,000”amesema Edith.

Kwa upande wa viongozi wa chuo kikuu cha Rwanda,Kiongozi makamu kwa wajibu wa maendeleo Dkt Charles Muligande ametangaza kwamba mabadiliko haya yatakapokubaliwa na wizara ya elimu na wengine husika yatakuwa umuhimu mno kwa wanafunzi na walimu ili kutimiza lengo la chuo.

Haya ni baada ya halmashauri ya elimu(HEC) kuzusha madai kwamba chuo kikuu cha Rwanda kilifanya mabadiliko kisiri pia kinyume  na sheria madai anayoyakana kwa kusema kwamba kulikuwa tafsiri potofu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top