SHERIA

Rwanda:Mahakamu kuu yealeza kutokuwa na uwezo wa kuhukumu kesi ya Joseph Nkusi

Mahakama kuu,kipande cha kuhukumu kesi za uhalifu wa nje ya mipaka kimeleza kuwa hakina uwezo wa kuhukumu kesi ya Joseph Nkusi anayeshtakiwa kuwa itikadi ya mauaji ya kimbali,uchochezi na kuzusha ghasia nchini.

Joseph Nkusi/Picha:Intaneti

Joseph Nkusi pamoja na mwanasheria wake,Me Antoinette Mukamusoni ameshangaa baada ya kusikia mkurugenzi wa baraza la hakimu wa kesi hii,Alice Umulisa kusema kwamba hawana uwezo wa kuhukumu kesi hii.

Mwendsha mashtaka,Eric Nkwaya ameleza kwamba mahakama hii inaweza kuhukumu kesi hii kwa kuwa mtuhumiwa alifanya uhalifu kupitia intaneti kupitia tovuti yake yenye maoni ya upinzani wa serikali kwa jina la Shikama, kwa hiyo ni uhalifu wa nje ya mipaka.

Kwa mjibu wa taarifa za VOA,Jaji Umulisa ameambia pande zote mbili kwamba haifai kuhukumu kesi ambayo hukumu yake haitakuwa na thamani na kuwa mahakama hii inahukumu uhalifu kama vile biashara ya binadamu na mengine kulingana na sheria.

Mtuhumiwa ameleza kwamba haya ni kumchelewesha na ukiukaji wa haki zake.

Haki chelewefu hazina thamani”ameleza Nkusi.

Joseph Nkusi, 55 ni mzaliwa wa Butare kusini mwa nchi, alikuwa mwalimu wa chuo kikuu,alitumwa na Norway mwezi Otoba 2016 baada ya kukosa hati rasmi za ukimbizi.

Jaji atatangaza kama ana uwezo ama hana uwezo wa kuhukumu kesi hii tarehe 26 October 2017.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top