HABARI MPYA

Rwanda:Kutokubaliana kwazuka kati ya uendesha mashtaka na mtuhumiwa wa mauaji ya kimbali kuhusu mawasilano na familia yake.

Kwa mjibu wa taarifa za BBC,Kutoelewana kumetokea kati ya uendesha mashtaka na mtuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994, Sous-Lieutenant Jean Claude Seyoboka, 51 (EX-FAR) anayesema kwamba alikosa namna ya kuwasiliana na mke na wana wake.

Mtuhumiwa ameleza kwamba anahitaji rukhusa ya kuongea na familia yake ili imtumie fedha za kulipa mwanasheria wake,Albert Nkundabatware na kuwa anahitaji kuwasiliana na shahidi wake.

Uendesha mashtaka umepiga marufuku ombi lake kwa kusema kwamba sababu zake hazitazuia kesi kuendelea na kumkumbusha Seyoboka kwamba yeye ni mfungwa hastahili fadhila hizi.

Sous-Lieutenant Jean Claude Seyoboka anatuhumiwa kuua na kubaka wanawake alipokuwa akishi mjini Kigali,eneo la Rugenge wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top