kwamamaza 7

Rwanda:Katibu mtendaji wa mji mkuu afungwa jela

0

Polisi imehakikisha taarifa za kumfunga jela katibu mtendaji wa mji mkuu Kigali,Eng.Didier Sagashya pamoja na mafisa wenzake wawili wakiwemo Merard Mpabwanamungu na Enos Twahirwa.

Msemaji wa polisi,ACP Theos Badege ametangazia The New Times kuwahawa wamefungwa ili kufanyiwa upelelezi  juu ya ushirikiano wa kuharibu hati za miradi ya ujenzi na kuwongeza kwamba watafika mikononi mwa muendesha mashtaka baada ya upelelezi kumalizika.

Msemaji wa polisi amesema”Watatu wanafanyiwa upelelezi kwa kuharibu ushahidi,kubuni ama kubadilisha hati”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya mkurungenzi wa halmashauri ya mji wa Kigali,Athanase Rutabingwa siku tatu kabla kutangaza kuwa Eng.Didier Sagashya alifukuzwa kazini juu ya makosa husika na kuharibu hati za miradi ya ujenzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kulingana na sheria za kuadhibu nchini Rwanda,makala yake 571 na 609 inaeleza kuwa uhalifu wa kuharibu ushahidi unaddhibiwa kufungwa jela miaka mitatu pamoja na kutoa faini ya Frw kuanzia Rwf 300,000 hadi miliyoni moja .Uhalifu wa kubuni ama kubadili hati  unadhibiwa kufungwa jela miaka mitano hadi saba pamoja na kutoa faini ya Rwf 300,000 hadi miliyoni tatu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Eng.Didier Sagashya alichakuliwa nafasi ya katibu mtendaji wa mji mwezi Februari 2017,Alikuwa mkurugenzi wa Ofisi kuu ya ujenzi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.