BURURUDANI

Rwanda:FIFA yakomesha uchaguzi wa kiongozi wa FERWAFA

Muungano wa mashirika ya kandanda duniani(FIFA) umekomesha uchaguzi wa kiongozi wa shirika la kandanda nchini Rwanda(FERWAFA) uliopangwa tarehe 10 September 2017.

Kiongozi wa FIFA,Ivantino(kushoto) akiwa pamoja na kiongozi wa FERWAFA(kuria),Nzamwita Vincent De Gaulle

FIFA imetumia FERWAFA barua ya kukomesha uchaguzi,ni baada ya moja mwa washiriki wa FERWAFA kuandikia barua FIFA wakisema kuwa maandalizi  ya uchaguzi huu  hayakufuatilia kanuni.

Barua hii iliyoandikwa na katibu mtendaji wa FIFA,Fatma Samoura inaeleza kuwa FIFA itanzisha upelelezi  na uchambuzi kuhusu yaliyomo ya barua iliyoandikwa na moja mwa washiriki wa FERWAFA.

Uchaguzi mwingine utafanyika baada ya siku 90

Haya ni baada ya taarifa za kuwa kuna  vuguvugu  katika uongozi wa FERWAFA yenye uhusiano na  matumizi ya fedha ya kiongozi wake,Nzamwita Vincent De Gaulle.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top