Connect with us

HABARI

Rwanda:Daktari alazwa hospitali ya saikolojia baada ya mahabubu wake kumuaga

Published

on

Kijana kutoka nchini Uganda kwa jina la Byaruhanga aliyekuwa daktari kwenye hospitali ya Gahini amepelekwa kwenye hospitali ya saikolojia ya Ndera kwa ajili ya kiwewe cha kuwa mpenzi wake amemuaga.

Haya ni baada yake kijana daktari kujengea mama wa kimwana wake nyumba ya kifahari,kuuza duka la dawa,kuuza ngo’mbe 22 ili kumpa chochote atakacho mpenzi wake.

Majirani wake wamesema kwamba wawili walikuwa kidole na pete lakini baada yake mama wa msichana kujengewa nyumba msichana kwa jina la Kamukama alimuaga.

Baada ya kisa hiki,Byaruhanga alitoweka wakati wa miezi 3, na kulala katika miti,amepatikana baada ya viongozi kumushawishi mpenzi wake,Kamukama kumpigia simu.

Byaruhanga ameonekana akiva nguo kukuu na kueleza kwamba haoni thamani ya maisha baada ya mpenzi wake kukata kufunga ndoa naye.

Alijaribu kujiua lakini wenzake wakamunusuru kisha akapelekwa kwenye hospitali ya saikolojia ili agangwe vilivyo.

.Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *