HABARI MPYA

Rwanda:Changamoto ambazo Rais Kagame hana budi kutatua kwenye mamlaka mpya

Mwalimu wa chuo na mtalaam kuhusu uchambuzi wa siasa,Dk. Christopher Kayumba amehoji kwamba Rais Kagame anapaswa kutoa suluhisho za changamoto mbili zikiwemo kusikiliza maoni ya wapinzani na kuwajibu kwa matendo, pia kusikiliza waliowahi kuwa”Inkotanyi” wenye nia ya kuomba msamaha.

Kwa mujibu wa taarifa za The East African,Dk.Christopher Kayumba ameleza kwamba haelewi namna ambavyo wanaolaumu serikali ya Rwanda kupitia ripoti na viombo vya habari vikubwa lakini upande wa serikali ukajibu kwa kutumia twitter tu.

Dk.Kayumba amendelea kwa kusema kuwa kunahitajika mwenendo wa kugawa uongozi,kusikiliza maoni ya wapinzani wenye thibitisho bila chuki na uongo.

Pengine,kutoa msamaha kwa waliokuwa “Inkotanyi” Dk.Kayumba amesema kuwa Rais Kagame hana budi kutoa msamaha kwa wale wanaouhitaji kwani serikali iliyotoa msamaha kwa walioshiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 haitashindwa kuwasamehe walioikomboa nchi kwa kosa dogo walilofanya.

Dk.Christopher Kayumba amesisitiza kuwa kutoa suluhisho za changamoto hizi ni jambo ambalo litaongeza wazi wazi urithi wa Rais Kagame hata baada yake kuondoka madarakani.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top