HABARI MPYA

Rwanda:Askofu wapiga marufuku utoaji mimba

Askofu wa dini ya wakatoliki wote nchini wamepiga marufuku utoaji wa mimba unaoruhusiwa na kanuni kwa kueleza kuwa hili ni mauaji ya mtu ambaye hana hatia na kuwa hakuna sababu yoyote inayomruhusu fulani kumuua binadamu,jambo linaloathiri jamii na nchi kwa ujumla.

Kupitia tangazo lao wemesema kuwa afya ya binadamu ni zawadi ya Mungu na kuwa haina budi kuheshimiwa, kulindwa  na kuwa utaoji wa mimba siyo suluhisho la tatizo bali linaharibu upendo na maisha ya familia.

Pia askofu wamewataka wowote husika na jambo hili hasa wanzisha sheria,madaktari na jamii kwa ujumla kutofanya lolote linaloweza kuharibu maisha ya binadamu tangu ujauzito.

Askofu wameweka mawazo yao kuhusu jambo hili wakati ambapo bungeni,tume ya mambo ya kisiasa hivi karibuni kumejadiliwa kanuni husika na utoaji mimba ambayo inaeleza wanaokubaliwa kutoa mimba kama vile mimba inayoathiri mjamzito ama mtoto,mimba ya watu wenye uhusiano wa karibu hadi kwenye cheo cha pili,mjamzito mwenye umri mdogo,aliyepata mimba kwa nguvu,aliyepata mimba baada ya kufunga ndoa bila hiari.

Katibu hali kwa wajibu wa katiba na sheria nyingine,Evode Uwizeyimana ameleza kuwa serikali inaunga mkono jambo hili  na kusisitiza kwamba utoaji mimba utatekelezwa na madaktari wanaokubaliwa na serikali.

Pamoja na haya,askofu wameleza kuwa wataendelea kijadiliana na serikali kuhusu jambo hili kwa kulinda haki za binadamu.

Isipokuwa ajili hizi za utoaji mimba unaokubaliwa na sheria,utoaji mwingine unadhibiwa kulingana na sheria.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top