HABARI MPYA

Rwanda yapiga marufuku ripoti ya shilika la haki za binadamu husika na kuwatesa wapinzani wake

Serikali ya Rwanda imekana mashtaka ya shilika la haki za binadamu,HRW husika na kuwatesa wapinzani wake baada ya uchaguzi wa rais mwaka huu.

Waziri wa mambo ya nje,Louise Mushikiwabo/Picha:Intaneti

Serikali ya Rwanda imekana mashtaka yaliyotangazwa na kiongozi wa HRW mwa Afrika ya kati,Ida Sawyer kupitia tangazo lake tarehe 29 Septemba 2017.

Kiongozi wa HRW mwa Afrika ya kati,Ida Sawyer

Kiongozi huyu alidai kwamba serikali ya Rwanda serikali ya Rwanda inatesa wapinzani na kuwa haitaki kusikiliza maoni ya wapinzan wake.

Kwa kujibu shutuma hizi,waziri wa Rwanda wa mambo ya nje,Louise Mushikiwabo amesema kwamba shilika hili halifanyi kazi yake vilivyo na kuwa linachanganya watu kuhusu Rwanda.

Ripoti ya awali ya HRW ilitaja watu iliyosema kuwa waliuawa na walinzi wa usalama ambao ni hai”amenena waziri Mushikiwabo.

Pamoja na hayo,serikali ya Rwanda hukana ripoti nyingi za  shilika la haki za binadamu tangu miaka ya awali kwa kueleza kwamba ripoti hizi ni uong’o mtupu.  

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top