BIASHARA

Rwanda yajitokeza kwenye nafasi ya pili kwa kutoa huduma bora barani Afrika

Ripoti mpya ya uchumi 2017/2018 inaonyesha kuwa Rwanda ina nafasi ya pili mwa Afrika naya 41 dunia nzima kwa kutoa huduma bora.

Mkurugenzi mkuu makamu wa bodi ya maendeleo(RDB),Bw Emmanuel Hategeka amesema kuwa hii ni hatua nzuri ila safari ingali ndefu katika utoaji wa huduma bora.

Emmanuel Hategeka amehamasisha watu binafsi kuboresha utoaji wa huduma katika kazi zao za kila siku.

Mkurugenzi wa mambo ya utalii wa RDB,Belise Kalisa ametangaza kwamba huu ni muda mzuri wa kutega masikio zaidi wateja wa bodi zinazotoa huduma ili kuridhisha mahitaji yao kwa kuwa huduma mbaya ni kizuizi cha maendeleo ya nchi.

Rwanda inasherekea wiki ya kutoa huduma bora,inafuata visiwa vya Mauritius kwa kutoa huduma bora barani Afrika.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top