HABARI MPYA

Rwanda yajikuta njia panda kuhusu kufungwa kwa waliomteka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame

Rwanda inajiuliza mengi kuhusu kufungwa kwa walioshiriki kumteka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame,Luteni Joel Mutabazi kwa kuwa huyu alikuwa kwenye orodha ya watu wanaowindwa na Interpol juu ya uhalifu aliofanya nchini Rwanda.

Rwanda inasisitiza kuwa Luteni Joel Mutabazi alikamatwa kulingana na kanuni za kimataifa na kukosoa namna ambavyo Rene Rutagungira anayeshtakiwa kuongoza kisa hiki alikamatwa akiwa baani mjini Kampala.

 

Rwanda pia inakosoa vitendo vya serikali ya Uganda kwa kuwa kuna mkataba wa kuwasilisha wafungwa kati  ya nchi hizi mbili.

Msemaji wa polisi ya Rwanda,ACP Theos Badege ametangazia The East African kuwa Rwanda ilifuata kanuni zote za polisi ya kimataifa,Interpol kwa kumkamata Luteni Joel Mutabazi.

Luteni Mutabazi alihukumiwa kufungwa maisha jela,kuondolewa vyeo vyake vyote baada ya kushtakiwa uhalifu wa mauaji na kuwaunga mkono wanamgambo wa FDLR na RNC.

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top