kwamamaza 7

Rwanda yaiomba Marekani msaada wa kupamabana na makundi ya kigaidi ya FDLR na RNC

0

Serikali ya Rwanda imeiomba serikali ya Marekani msaada wa kupambana na makundi ya waasi wake wakiwemo FDLR na RNC.

Ujumbe huu umetolewa na Mkurugenzi wa Maseneta, Bernard Makuza katika mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Rwanda, Peter Vroom.

“  Tumemuambia kuhusu makundi ya kigaidi katika  haya maeneo. Bila kuficha kuna FDLR na makundi mengine yanayojigamba wizi. Tumemuambia hatuwezi kukaa kimya kwani usalama wan chi fulani ni kama wa nyinigine.” Seneta Makuza ameambia watangazaji baada ya mazungumzo.

Pia Makuza ameweka wazi kwamba ameiomba Marekani kutoa msaada katika mambo ya kuwakamata watuhumiwa wa mauaji ya kimbali dhidi ya Watutsi.

Hata hivyo, Makuza amesema, Balozi Vroom hakusema mengi kuhusu itakachofanya Marekani kuhusu suala la usalama.

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.