Rwanda imeamua kufunga mipaka yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) juu ya Ebola.

Uamuzi huu ni baada ya mgonjwa wa pili kufariki Mjini Goma, karibu na mpaka wake na Rwanda.

Wakazi wameeleza wameshanga kufika kwenye mpaka na kukataliwa kingia nchini Rwanda.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Gisenyi, Luteni Kanali Dkt. William Kanyankore amehakikisha taarifa hizo.

“  Ni ukweli mipaka imefungwa, tangazo linaloeleza mengi litapatika, subiri.” Amesema Dkt. William Kanyankore

Hata hivyo, wakazi wamesema ni hali inayohatarisha kazi zao za kila siku wanazofanyia Mjini Goma.

Kwa sasa, mgonjwa wa tatu amepatikana tena Mjini Goma.

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.