kwamamaza 7

Rwanda:  Waziri aunga mkono uamuzi wa SADC kuikatalia Burundi kuwa mshriki

0

Waziri Makamu wa Mambo ya Nje kwa Wajibu wa Shilika la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Amb. Olivier Nduhungirehe amesema Burundi itanufaika kutokuwa mshiriki wa Shilika la Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Siku chache zilizopita, SADC ilikana ombi la Burundi kuwa mmoja mwa washiriki wake.

Mkuruegenzi wake, pia Rais wa Namibia, Hage Geingob alipokuwa katika ziara yake ya kikazi nchini Tanzania, aliweka wazi kuwa Burundi haijatimiza mahitaji yote kukubaliwa kushriki katika SADC.

Alisema kuwa hali ya demokrasia nchini Burundi haijaeleweka nchini Burundi.

Akitoa hoja kuhusu uamuzi huu, Amb. Nduhungirehe, kupitia Twitter amesema “ Hata inavyoonekana, uamuzi wa SADC unaweza kunufaisha Burundi. Itapata fursa ya kuimarisha muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufanya wajibu wake vilivyo.”

Ni mala ya pili Burundi kukataliwa kuwa mshiriki wa SADC. Sababu ni kuwa haijatoa suluhisho kwa masuala ya kisiasa yaliyomo nchini humo tangu mwaka 2015.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.