kwamamaza 7

Rwanda: Watu wanaotamka Kinyarwanda washambulia na kuwaua watu wawili kusini

0

Watu wanaotumia lugha ya Kinyarwanda jana usiku wa manane wameshambulia  tarafa ya Nyabimata wilayani Nyaruguru kusini mwa Rwanda na kuua watu wawili,kujeruhi sita,kuiba mali na  kuteka nyara watu wengine.

Kiongozi wa baraza la washauri wa tarafa ya Nyabimata, Fidele Munyaneza ambaye ni mmoja mwa waliojeruhiwa ameeleza vyombo vya habari kuwa hawa walikuwa wakitamka Kinyarwanda.

“ Mmoja amekuja na kuniuliza kama mimi ni kiongozi nikasema hapana. Aliniambia nikimbie kisha akanipiga risasi kwenye mguu na kwa mkono.Walikuwa wakitamka Kinyarwanda”

Hawa watu wenye silaha wamechoma gari la Katibu mtendaji wa tarafa ya Nyabimata, Vincent  Nsengimana aliyejeruhiwa mno.

Gari la kiongozi lililochomwa

Pia, Wameiba mali za wakazi na kujaribu benki ya SACCO kijijini huko.

Haya ni baada ya siku chache watu wawili kupigwa risasi na kuuawa hapo hapo katika hii wilaya ya Nyaruguru.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.