kwamamaza 7

Rwanda: Watoto saba walioterekezwa maishani magumu waiomba serikali msaada

0

Watoto saba wana wametangaza kusihi katika maisha magumu wakati baada ya baba yao kufungwa jela mwaka 2009 na mama yao kuwaterekeza mnamo mwaka 2015.

Mtoto mwenye umri mkubwa baadhi yao, Eulade Udahemuka,21, ameambi a Gazeti la Bwiza.com hali ya maisha yao lilipomkuta Kijijini kwao Kabasanza, Kata la Gihara, Tarafa la Runda Wilayani Kamonyi Kusini mwa Rwanda.

Amesema baada ya kubaki bila mzazi mmoja, Udahemuka amesema alianza kuwatunza kaka zake wawili na dada zake wanne akiwa na umri wa miaka 17. Amesema wakati huo alikuwa mwanafunzi kifato cha nne.

Amesema familia yake ilipatiwa cheo cha tatu maarufu kama ‘Ubudehe’, jambo linalowazuia kupata msaada wa serikali. Cheo hiki kwa kawaida hupatiwa watu wenye uwezo.

“  Nina miaka 21. Ni jukumu langu kuwatunza ndugu zangu sita tangu nilipokuwa katikakidato cha nne, shule la sekondari. NI vigumu kwangu kwani sina kazi. Nafanya kazi za kawaida tu. Ni kwa Mola tu kuweza kutimiza hili.”

Alivyotuterekeza mama mzazi

Ameoambia Bwiza.com kwamba waliamka siku moja mwaka 2015 na kujikuta mama mzazi wao amekwenda mahali ambapo hawakujua.

Baada ya hilo walishi katika hali ngumu ya maisha na nyumba yao ilibomolewa na mvua kali mwaka 2018.

Akijibu kama aliwahi kuomba viongozi msaada, Udahemuka amesema viongozi wa ngazi za chini wanajua suala lao laikini hawajawasaidia lolote.

“  Kuna wakati ambapo ndugu zangu wanakosa mbinu za kufika shuleni. Wanakosa hata na mahitaji ya msingi kwa masomo yao.”

Ameeleza Mnyarwanda, Venuste Nshimiyimana ambaye anaishi nchini Uingereza kwamba anawasaidia kulipa kodi la nyumba, chakula na karo kwa dada yake mmoja anayesoma shule la sekondari.

Josiane Murebwayire, 15,  ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza, shule la sekondari, amesema masomo yake yanakabiliana na changamoto la kutoweza kupata mahitaji yote shuleni na nyumbani.

“  Maisha ni magumu kwa kuwa sina wazazi. Siwezi kupata mahitaji yote.” Ameambia Bwiza.com

Nduguye, Claudine Umutesi ameongeza “ Tunakabiliana na maisha magumu, siwezi kupata ninayohitaji.”

Wanafamilia hawaitowi msaada 

Udahemuka amesema mama mzazi wao alikuwa hana mwanafamilia yeyote kwani wote waliuawa wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Watutsi mwaka 1994. Amesema hawajapata msaada kutoka wanafamilia kwa upande wa baba yao.

Mtangazaji, Venuste Nshimirimana  amesema alijua familia hii kupitia rafiki yake, Jean Leonard Karuranga.

“ Ni [ Karuranga]  rafiki yangu miaka 30 iliyopita. Aliniambia kuna watoto wanaohitaji msaada. Niliongea na Eulade. Niliongea na ndugu ze wote Siwezi kukwepa sauri ya upendo. Nawajua kila mmoja kupitia sauti. Nilihisi kuwasaidia ni kama kusaidia Mungu.” amesema

“Nitaungana mkono na viongozi wa ngazi za chini kuwajengea nyumba. Karuranga alisha chora muonekano wa nyumba hiyo. Tunasaburi kiongozi wa kijiji kuhusu hiIi kwani anajua suala la wataoto hao. Kuna imani kwamba tutatimiza lengo letu.”

Hata hivyo, Udahemuka anawanyoshea kidole viongozi kwa kutia pamba masikioni kuhusu tatizo la familia yake.

“ Viongozi walijifanya hawatuoni. Wangeliwasiliana na viongozi wengine hata tupate makazi.” amesema

Pamoja na hayo, Eulade Udahemuka anaungana mkono na Laurence Mukamurigo kuwasaidia ndugu ze kuendelea na maisha.

Ameitaka serikali kuwapa msaada wa bima ya afya, makazi na mahitaji mengine.

Kwa upande mwingine, Bwiza.com imejaribu kuwasilaiana na Katibu Mtendaji wa Tarafa la Runda lakini haikufua dafu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.