kwamamaza 7

Rwanda: Wapinzani wanahitaji nafasi katika baraza la mawaziri

0

Chama cha upinzani nchini Rwanda, Democratic Green Party of Rwanda (DGPR) kimeweka wazi kwamba kinataka kuwa na nafasi  katika baraza la mawaziri.

Kiongozi wake na Mbunge, Dk. Frank Habineza amesema kwamba ombi lao linawezekana kutokana na kuwa ni haki inayotolewa na katiba ya nchi.

Kwenye mazungumzo na gazeti la Bwiza.com, amesema ombi hili  ni la wanachama wote kutoka mkutano wa wanachama mwezi Machi 2019.

“  Ni ukweli kwamba chama chetu kinataka nafasi ya uwaziri katika baraza la mawaziri. Ni ahadi yetu kwa wananchi tulipokuwa katika shughuli za kura ya urais mwaka 2017. Tulikuwa tunataka kuongoza baraza la mawaziri. Tunahitaji hili kama inavyoturuhus sheria.” Habineza amesema

“ Wanachama wanataka tuwasiliane na seneti kwa kuwa ni wajibu wake. Jambo hili linajadiliwa laikini uamuzi wa mwisho ni wa Rais. Tuna imani kwamba ataamua vilivyo kwani anatii sheria.” ameongeza

Kwa muijibu wa Katiba ya Rwanda, chama ambacho kinawakilishwa bungeni, kinaweza kuwa na nafasi katika baraza la mawaziri. Kwa hiyo, DGPR wanasema kuna imani watapatiwa nafasi hii.

“ Ni wajibu wa Rais wa Jamhuri kufanya hili. Ndiye ambaye anawachagua mawaziri. Lakini serikali ina nafasi nyingine kama vile, Makamu waziri, mabalozi na nyingine.”

Rwanda ilikubali rasmi DGPR ni chama  mwaka 2009. Hiki chama kilijulikana mno wakati wa uchaguzi ambako kilikosoa   chama tawala, RPF-Inkotanyi kuhusu mfumo wa uchaguzi nchini.

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.