Viongozi wa kambi ya wakimbizi ya kiziba wilayani Karongi,magharibi mwa Rwanda wametangaza kuwa 15 asili  ya DR Congo ndio waliouawa  80 walijeruhiwa pamoja na 30 kutoweka baada ya siku tatu za kufanya maandamano kuanzia   terehe 22 Februari 2018 kwenye makao ya shilika la Kimataifa la kuhudhumia wakimbizi(UNHCR).

Hawa Viongozi wametangazia Sauti ya Marekani,VOA kuwa hata wale waliofariki hawakuzikwa vilivyo kwa kuwa walizikwa na wakazi wengine  waliokuwa kwenye kazi za kijamii kwa jina’Umuganda’ baada ya shinikizo la serikali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ndugu ya aliyefariki ameeleza” Haikuwa kawaida ya kuzika watu, serikali ndiyo iliyofanya hili. Kwa sasa sikubali kuwa nilimzika ndugu yangu”

“Ilikuwa kama ni tukio la kutengeneza barabara,sisi tulisimama tu na kuangalia,hatukuzika watu wetu” ameongeza

Kiongozi wa hii kambi,Maombi Louis Mbangutsa ameeleza hawajui kwamba  wangali hai waliotoweka

“Kuna watu karibu 30 ambao familia zao haziwaoni hata gerezani.Tunafikiri kuwa waliuawa”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande mwingine,Serikali ya Rwanda kupitia waziri wa majanga na wakimbizi(MIDIMAR) De Bonheur Jeanne d’Arc amewaomboleza waliofiwa na kuwalaumu viongozi wa kambi kwa kueleza kwamba  ndio chanzo cha yaliyotokea

“Kwa niaba ya serikali ya Rwanda,tumesikitishwa na yaliyotokea ila tumesikitishwa na uamuzi wenu wa kusikiliza ushauri mbaya wa viongozi wao”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wakimbizi asili ya DR Congo 17 ,000 wanaishi kambi ya wakimbizi ya Kiziba tangu mwaka 1996.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.