HABARI MPYA

Rwanda-Ufaransa:Wanadiplomasia kukutana kisiri mjini Kigali

Wanadiplomasia wa Ufaransa na wa Rwanda wanatarajia kukutana kisiri mjini Kigali mwezi ujao kwa mujibu wa taarifa za Jeune Afrique.

Rais Kagame na mwenzake,Emmanuel Macron

Taarifa hizi zinasema kuwa haya ni baada ya afisa kwa wajibu wa mambo ya Afrika katika wizara ya mambo ya nje nchini Ufaransa,Remi Mercheaux na mshauri makamu kwa mambo ya Afrika katika ikulu,Marie Adouard kukutana na waziri wa mambo ya nje nchini Rwanda,Louise Mushikiwabo mwezi huu.

Pengine,ni mkutano wa siri kati ya Rais Paul Kagame na Rais Emmanuel Macron uliozungumza kuhusu mabadiliko yatakaytokea kwenye Umoja wa Afrika wakati ambapo Rais Kagame atakuwa kiongozi wake mwaka uajao 2018.

Kunatarajiwa kwamba Rais Kagame atahudhuria mkutano kuhusu amani ana usalama tarehe 13 Novemba 2017 itakayongozwa na Senegal na Ufaransa.

Kwa mjibu wa Jeune Afrique hizi ni dalili za ushirikiano mzuri kati ya Rwanda na Ufaransa,nchi ambazo ushirikiano wa kidiplomasia wake ulichafuka kuanzia mwaka 1994.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top