kwamamaza 7

Rwanda: Serikali yafukuza Warundi 115 walioingia nchini kinyume na sheria

0

Serikali ya Rwanda jumamosi imewarudisha kwao  Warundi 115 walioingia nchini kinyume na sheria.

Hawa wamekaribishwa na vingozi wilayani Ntega, mkoa wa Kirundo kupitia mpaka wa Akanyaru.

Hata hivyo, waliofukuzwa wameeleza kuwa inawezekana kufukuzwa kwao ni sababu za shambulizi lililotokea wilayani Nyaruguru karibu na Burundi.

Wengi mwa hawa  95  wanaishi wilayani  Ntega, wengine Ngozi na Muyinga

Hawa Warundi wametangazia Sauti ya Marekani kuwa walikuwa wakifanya kazi za kawaida nchini Rwanda na kuwa Rwanda imewataka kurudi kwao kutafuta vitambulisho.

Miongoni mwao kuna waliotangaza kuwa walipigwa kabla ya kuondoka nchini Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.