kwamamaza 7

Rwanda: Mzazi afungwa kwa kutuhumiwa kubaka bintiye wa miaka 14

0

Mwanaume Wilayani Ruhango, Kusini mwa Rwanda amekamatwa juu ya tuhuma kwamba alikuwa akimbaka bintiye wa miaka 14 baada ya kufarakana na mkewe.

Huyu mwenye umri wa miaka 40 alikamatwa jana tarehe 8 Mei baada ya mwanawe kusambaza habari kwamba anafanya mapenzi na baba yake na kuwa imekuwa kawaida.

Katibu Mtendaji kijijini anakoishi mtuhumiwa, Grace Umuhire ameambia vyombo vya habari nchini Rwanda kuwa mtoto aliwambia watu mbali mbali kuhusu kisa hiki lakini hawakumuamini.

“ Alimuambia nyanyaye, mama wa baba yake na wa mama yake lakini walitia pamba masikioni. Alipowambia marafiki wa baba yake walidhani anataka kumharibia jina baba yake.”

Mtoto amepelekwa Hospitalini ili kupima hali ya maisha yake na baba yake amekamatwa na Ofisi ya Upelelezi nchini Rwanda.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.