kwamamaza 7

Rwanda kuzungumza na Marekani kuhusu marufuku ya kafa ulaya

0

Waziri wa Biashara na Viwanda Vincent Munyeshyaka ametangazia Radiyo Flash kwamba itawezekana kuzungumza na Marekani siku 60 za usoni juu ya uamuzi wake wa kuikomesha Rwanda katika mkataba wa AGOA hata kama Rwanda hainufaiki mno.

“Biashara yetu na Marekani katika AGOA haiko hata asilimia nusu,wakionyesha wanalotaka na uamuzi wao,nafikiri kuwa wakati wa miezi miwili tukiona kuna athari,tunaweza kukaa tukazungumza na ninawaza watasikiliza maoni yetu”

Waziri Munyeshyaka ametangaza haya baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuweka wazi kuwa  bidhaa kutoka Rwanda zitapigwa marufuku nchini Marekani kutokana na kuwa  Rwanda  inaendelea kuwa kipingamizi cha  sela za kiuchumi na uwekezaji wa Marekani  kwa kupiga marufuku kafa ulaya.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Trump alisema kwamba hili ni kinyume na utekelezaji  wa mkataba wa AGOA , makala yake ya 104.

Mkataba wa AGOA ulianzishwa na Rais wa Marekani Bill Clinton mwaka 2000 na kutiliwa saini na nchi 38 zikiwemo Rwanda.Huu mkataba unalenga kuzirahisishia nchi za chini ya jangwa la Sahara kuuza baadhi ya bidhaa zake bila kodi nchini Marekani.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.