kwamamaza 7

Rwanda: Kunatumiwa kamera kupima ugonjwa wa Ebola

0

Serikali ya Rwanda inatumia kamera kwenye mpaka na DRC kupima watu wenye ugonjwa wa Ebola.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Gisenyi, Luteni Kanali William Kanyankore amesema kamera inapima mtu mwenye homa nyingi katika kundi la watu wengi.

“ Tumemaliza kufunga kamera tatu zenye uwezo mkubwa wa kupima homa kwa watu wengi mala moja” amesema Kanyankore

Amesema hatua hii imechukuliwa kutokana na kuwa ilikuwa ikichukua muda mrefu kumpima kila mtu.

Diwani wa Wilaya ya Rubavu, Gilbert Habyarimana amesema wanafanya juu chini kuzuia wananchi wanaotumia njia ziziso za mpaka ili wapimwe uginjwa wa Ebola.

Miezi kumi imepita ugonjwa wa Ebola ukiangamiza raia nchini DRC. Kwa hiyo, Rwanda imekaa tahadahari juu ya ugonjwa huu.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.