HABARI

Rwanda kufanya maandalizi ya nishati ya Nyuklia

Rwanda inatarajia kuanzisha mradi wa kutumia nishati ya nyuklia kwenye sekta mbalimbali zikiwemo umeme,uganga,ukulima na uchimbaji wa petroli.

Kupitia waziri makamu wa wizara ya miundo mbinu kwa wajibu wa nishati,Germaine Kamayirese,kunatarajiwa kuanzisha matumizi ya nishati ya nyuklia kwa kiwango cha juu.

Tumeisha kuwa tayari kutumia nishati ya nyuklia,tunaweza kuanzisha viwanda vya umeme, kutibu  kansa kwa namna ya kisasa na mengine(radiotherapy)”amesema Waziri Kamayirese.

Mkurugenzi wa bodi itakayofanya ufuatiliaji wa matumizi ya nishati ya nyuklia,Major.Patrick Nyirishema ametangazia Tv 10 kuwa wanajianda vilivyo kujitayarisha  kama vile  kuweka sheria,uwezo na kujenga ushirikiano na ofisi nyingine kwa matumizi bora ya nishati hii.

Hata kama Rwanda inatarajia kutumia nishati ya nyuklia,jambo hili litachukua muda mrefu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top