kwamamaza 7

Rwanda kucheza na Sudan leo wakijiandaa kuikuta Uganda mwishoni mwa wiki

0

Timu ya Taifa ya Soka ya Rwanda inachuana na Timu ya Sudani katika mchezo wa kujipima nguvu ikiwa timu hizi mbili zinajiandaa mashindano michezo ya raundi ya tatu ya kufuzu Kombe la Afrika kwa wachezaji wa Nyumbani.

Mchezo kati ya Rwanda na Sudani utapigwa Jumatatu ya leo kwenye uwanja wa Kigali ulioko Nyamirambo mwendo wa saa tisa na nusu.

Timu zote zinajipima nguvu ikiwa zinajiandaa michezo ya raundi ya tatu ya kufuzu kombe la Afrika la mataifa kwa wachezaji wa nyumbani. Timu ya Rwanda yakwenda kucheza ikiwa inajiandaa kupambana na Timu ya Uganda (the cranes) mwishoni mwa wiki hii. Pengine timu ya Sudan inajiandaa kuwakuta Etiopia katika raundi hiyo hiyo.

Rwanda ambayo inakutana na Sudan leo hii inajiandaa safari ya kwenda Uganda kupambana na timu hiyo mahasimu juma tano hii. Mchezo wa Uganda na Rwanda utapigwa tarehe 12 kwenye kiwanja cha St. Marys Kitende ambako mechi ya marudiano itapigwa wiki moja baadaye.

Timu itakayokuwa mshindi kwenye mechi hizo mbili itafuzu tiketi ya kushiki katika mashindano ya CHAN ambayo atafanyika mwaka ujao nchi Kenya.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.