Connect with us

HABARI

Rwamagana:Wanaume hukaa kimya baada ya kupigwa na wanawake wao

Published

on

Wanaume tarafani Kigabiro,wilayani Rwamagana wameweka wazi kuwa wanakaa kimyaa wanapopigwa na wanawake wao kwa kuogopa kuonea na wanaume wenzao.

Mkazi tarafani Kigabiro ameeleza kwamba kuna wakati fulani ambapo wanawake wanakiuka haki za wanaume wao kwa kuwapiga.

Kijijini kwetu kuna wanawake wanaopiga wanaume wao,kuna mmoja ambaye alipiga mayowe baada ya mwanamke wake kumpiga sana”ameeleza.

Mwanamume ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema kuwa wanapigwa ila wanaona aibu kufunguka hadharani kuhusu  kisa hiki.

Huyu amesema”Wanaume wengi tunapigwa ila wanaofunguka huwacheka kwa kusema kuwa ni mabwege”.

Kwa upande wa wanawake mmoja wao,Xaverine Muhawenimana ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nyagasenyi ametangaza kwamba kuna wanawake wanaopiga wanaume wao ila ni chanzo cha kuwa hawelewi vizuri suala la usawa wa jinsia.

Msemaji wa polisi mkoani Mashariki,CIP Theobald Kanamugire,amehamasisha wanaume kufunguka kuhusu ukiukaji wa haki wanaofanyiwa na wanawake ili sheria zifuatiliwe.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na Twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *