kwamamaza 7

Rwamagana: Waibuka na tabia ya kutapeli watu kwa kuwanyanganya fedha wakitumia harusi

0

Raia wa Rwamagana wanalalamikia tabia mbaya iliyozuka siku hizi ya kuandaa harusi kukilengwa kuwanyanganya watu fedha na mwishowe harusi zisifanyike na wanaharusi wakatoroka.

Mojawapo wa raia hao wanasema yaiko tena rahisi kumwamini yeyote akikualika kushiriki harusi yake.

Mukamuhigirwa Salim ambaye anaishi mjini Rwamagana asema kwamba na hata kushiriki mwito wa maandalizi ya harusi kwa sasa inahitaji kujitahadhari kwa kuwa kumekuwa kukiandaliwa harusi nyingi na mchango wa kifedha ukatolewa na akaishia hapo harusi zisifanyike.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“tumekuwa tukitarajia kushiriki harusi iliyokuwa imepangwa kufanyika majuzi jumamosi na tulikuwa tumeitika mwito wa maandalizi na hata mchango ukatolewa lakini tulishangaa kusikia harusi haitafanyika.

Kuna mwanamke ambaye ni mwanachama mwenza wa shiriki chetu cha kujiendeleza aliyeandaa harusi na kutualika na hata miito ya maandalizi ikafanyika halafu michango ya kifedha ikatolewa lakini alituambia mwishowe kwamba harusi hiyo haitafanyika. Huenda atakayetaka mtaji wa kuanza biashara atalazimika kuandaa harusi!!” asema

Mojawapo wa raia wananasema kuwa ujanja huu unahusiana na wadanganyifu wanaotaka kuwanyanganya watu fedha zao.

Katika mwezi huu wa Julai tu kumekuwa na harusi mbili zilizoandaliwa na kutofanyika na hata wanaharusi kutoroka.

Kumekuwa kukitarajiwa kufanyika harusi ya kijana mmoja wa tarafa ya Mwurire aliyekuwa akijiaandaa kufunga ndoa na msichana wa tarafa ya Gahengeri lakini baada ya Kijana huyo kukamatwa kwa makosa ya uizi harusi hiyo imevunjika na msichana akakimbia eneo hilo na hakuna anayejua alipo.

Kumekuwa kukitarajiwa pia harusi nyingine kufanyika katika tarafa ya Kigabiro sehemu za Cyanya Jumamosi tarehe 30 Julai lakini hiyo hiyo pia haikufanyika na hakuna anayejua alipo aliyekuwa akitarajiwa kuwa Bi harusi.

Kuna harusi nyingine iliyokuwa ikitarajiwa kufanyika mwezi Machi na kushindwa na hiyi ilizua kutoelewana kwa mama mzazi wa msichana na mama wanachama wa shirika wenzake wakidai kurudishwa fedha walizochangia kwenye harusi hiyo.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.