HABARI

Ruhango:Njaa yakumba wakazi baada ya uongozi kuwapokonya  mashamba yao

Wakazi wa tarafa ya Ruhango waliomiliki mashamba kwenye bwawa la Cyihene wametangaza kuwa wanakumbwa na njaa baada ya serikali kuwapokonya mashamba yao na kumpa mwekezaji kwa Jina la Deo Rutayisire mwaka 2010.

Mmoja mwa wakazi,Sephanie Nsengiyumva amesema kuwa hili ni ukiukaji wa haki za binadamu kwa kuwa walipokonywa mali ambayo serikali iliwapatia mwaka 1971.

Mwenzake amekamilisha haya kwa kusema kuwa linalowakera sana ni namna ambavyo mwekezaji alikuja kwa kuharibu mazao yao yakiwemo viazi vikuu bila fidia.

Wakazi hawa wamendelea kusema kuwa hili ndilo chanzo cha njaa inayowakumba wakati ambapo mwekezaji aliacha bwawa hili bila kuanzisha mradi wowote isipokuwa shimo mbili za kufugia samaki tu.

Diwani wa wilaya ya Ruhango,Francois Xavier Mbabazi ametangazia VOA kuwa wanajianda kurudishia bwawa hili kwa wakazi kwa kuwa mwekezaji alishindwa kutoa matokeo yaliyokuwa yakitalajiwa.

Bwawa hili la Cyihene lina ha 80.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top