HABARI MPYA

Ruhango:Maisha ya bikizee Karuhimbi aliyewanusuru Watutsi 100  yangali hatarini

Maisha ya Zula Karuhimbi mkazi wa tarafa ya Ruhango,kusini mwa Rwanda anayesema kuwa ana umri wa miaka 106, ambaye aliwanusuru Watutsi 100 wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 yangali hatarini kutokana na wivu wa majirani wake.

Zulfat Niyigena ambaye anaishi pamoja na Karuhimbi ametangaza kuwa hawapati hata lepe la usingizi kutokana na woga wa uvamizi wa majirani wao .

“Sipati usingizi,nikisinzia majirani  wanaweza kuibomoa nyumba hii na kutuua,wanafikiri kuwa shangazi ana fedha nyingi”

Kwa sasa sipati usingizi kutokana na kulinda usalama wake,macho yananiuma kwa kutosinzia.Majirani hawana furaha ya mafanikio yake “ameongeza

Woga huu unatokana na namna ambavyo majambazi  walivyoshambulia numba aliyojengewa na serikali na kumuiba vifaa vya nyumbani alivyopatiwa na viongozi wa tarafa siku zilizopita.

Bikizee Karuhimbi  ni mmoja mwa watu waliovishwa mdali na Rais Kagame mwaka 2007 kwa wema wake wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 alipowaficha Watutsi 100  nyumbani kwake.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top