kwamamaza 7

Ruhango: Wataka Warundi walioshiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Watutsi wakamatwe

0

Wanachi Wilayani  Ruhango, kusini mwa Rwanda wameitaka serikali iwakamate halafu wasimame kizimbani Warundi walioshiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Watutsi mwaka 1994 katika eneo hili.

Wanaoshtakiwa ni Warundi waliokuwa wakimbizi wakati huo panapoitwa Ntongwe.

Mmoja mwa wananchi, aliyemusurika mauaji ya kimbali, Iragena Jean Baptiste ameambia chombo cha habari Igihe.com kwamba  hawa Warundi hawajakamatwa ili kuulizwa waliyofanya mwaka 1994.

Kiongozi wa Shirika linalopambania faida za walionusurika mauaji ya kimbali (IBUKA) Wilayani Ruhango, Narcisse Munyanziza amesema suala la Warundi walioua Watutsi linahitaji kufuatiliwa vilivyo.

“ Kuna suala la Warundi walioua ndugu zetu wilayani humu. Tuna tumaini kwamba serikali yetu itafanya lolote kuhusu hili jambo, haitashindwa.  Ni bahati njema kujua inapofika kutupa haki kuhusu Warundi walioua watu wilayani Ruhango.” Narcisse amesema

Waziri Makamu wa Mambo ya Nje, Olivier Nduhungirehe amesema hakusema jambo hili linafika wapi ila amewapa moyo kwamba serikali ya Rwanda itafanya lolote husika.

“ Serikali ya Rwanda itafanya ufuatiliaji wa mauaji aliyofanywa na Warundi huku Kinazi, wilayani nap engine.” Waziri Nduhungirehe amesema

Hata hivyo, Ofisi ya Uendesha mashtaka nchini Rwanda ilitangaza si rahisi kuwakamata watuhumiwa kutokana na kuwa majina yao yote hayajulikani.

Pia Warundi wanashtakiwa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Watutsi Tarafa ya Rilima, Wilayani Bugesera, Mugina, Wilayani Kamonyi na Wilayani Gisagara.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.