HABARI

Rubavu:Wazazi wahamasishwa kupiga marufuku ukiukaji wa haki za watoto

Viongozi wa wilaya ya Rubavu,kaskazini magharibi mwa nchi wamehamasisha wazazi kupiga marufuku vitendo vya ukiukaji wa haki za watoto kama vile kubeba kuni,uchuuzi wa muwa,kuchimba mchanga na kazi nyingine za sulubu.

Kauli hii viongozi wameitoa jana kwenye sikukuu ya watoto,viongozi wamesema kuwa wazazi hawana budi kulea watoto wao vizuri.

Diwani makamu kwa wajibu wa mambo ya kijamii,Marie Grace Uwamapayizina ameleza kuwa kuna ukiukaji wa haki za watoto kwa kuwapatia kazi za sulubu hasa tarafa ya Nyundo kama vile kuchimba michanga,kazi ambazo zinawazuia kundelea na masomo yao.

“Tunahamasisha wazazi kutopatia kazi za sulubu watoto wao,kazi hizi huazuia watoto kuendelea na masomo yao”ameteta Diwani Marie Grace.

Baadhi ya wazazi wametangazia RBA kuwa ukiukaji huu wa haki za binadamu husababiswa na ufukara na kuwa wameisha zinduka kuhusu haki za watoto ambazo wataanza kutii.

Afisa wa shilika la Right to play,Valens Ndayavuze amesema kuwa pamoja na shilika la kimataifa la kuhudumia watoto,UNICEF wataimarisha mambo ya haki za watoto kwa kuanzia makundi madogo ya watoto wenyewe ili watoto hawa waweze kujua na kuuliza viongozi nini kinachoenda mbele.

Pamoja  na haya,Viongozi wa wilaya ya Rubavu wamefanya maandalizi ya kampeni ya kupiga marufuku ukiukaji wa haki za watoto ijumaa wiki hii.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top