HABARI

Rubavu:Wamiliki wa mashamba kwenye mlima wa Rubavu walalamikia mazao waliyoamuriwa kupanda

Wakazi wa tarafa ya Rubavu na Cyanzarwe wanaomiliki mashamba kwenye mlima wa Rubavu hawakubaliani na uongozi wa wilaya baada ya kuamurisha kupanda miti kwenye ardhi wanayotaka kupandia mazao mengine ya kawaida.

Mmoja wao,Mussa Saidi amesema kwamba hawakukubaliana na uamuzi wa wilaya kwani ni kinyume na ahadi ya Rais wa jamhuri Paul Kagame aliyewakubali kulima mashamba yao.

Hatukufurahia uamuzi  ule,tutakula miti?” Mussa Saidi amesema.

Kwa upande wa uongozi wa wilaya ya Rubavu,afisa wa wilaya kwa wajibu wa misitu na maliasili,Jacques Ndikubwimana ameleza kwamba wakazi hawa wanatelekeza uamuzi uliochukuriwa kwa ushirikiano na waliokuweko kwa niaba yao.

Kiongozi huyu amesisitiza kuwa uamuzi huu ni kwa lengo la kulinda mji wa Gisenyi mmomonyoko.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top