HABARI

Rubavu:Wakazi wanaotibiwa kwenye zahanati ya Karambo walalamikia huduma mbaya

Wakazi wanaotibiwa kwenye zahanati ya Karambo,tarafa ya Kanama wameweka wazi kuwa wanakosa dawa na mara nyingine hununua kwenye duka la dawa.

Mmoja wao asiyetaka kutajwa jina ameleza kuwa hawajui sababu ya kulipa fedha za bima ya afya ikiwa hawapati dawa.

Uhaba wa dawa unasisitizwa na daktari mmoja wa zahanati,Verena Ntakirutimana ambaye amesema kuwa mala nyingi duka lao huwa linahifadhi ‘Paracetamol’ tu.

Amesema”Twamaliza mwezi wote wa Agosti bila kupata dawa”.

Kiongozi kwa wajibu wa mali wa hazanati,Blandine Bakiza yakana madai haya kwa kuonyesha Ankara za kila mwezi za kununua dawa.

Kwa upande mwingine ,mkurugenzi wa zahanati ya Karambo,Fidele Ngirumpatse amesema kwamba kuliwahi kutokea matatizo haya kwa ajili ya uhaba wa fedha za bima ya afya.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top