kwamamaza 7

RUBAVU: WENYE MAMLAKA YA KUHIFADHI MISITI WALALAMIKIA KUONEWA NA WACHUNGAJI NG’OMBE

0

Wajasiriamali wenye mamlaka ya  kuhifadhi misitu huko wilayani Rubavu, watangaza kuwa wanasumbuliwa sana na wachungaji ng’ombe ambao wanaharibu miti ya misitu hiyo na hata kuwaonea kwa kuwapiga.

Wajasiliamali hao wenye mamlaka ya kihifadhi misitu matarafani Rubavu, Nyakiriba, Kanama na Kanzenze, Nsengiyumva Julien,wamesema kuwa wachungaji hao hasa wa ng’ombe hukata miti , kuwachunga ng’ombe kwenye miti midogo pamoja na kuiharibu miti ambayo mara nyingi huwa imepandwa na raia kwenye shughuli za umma, na mwenye kulalamikia hilo hupigwa na kujeruhiwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Amesema “mimi nilipigwa na kukatwa na panga kichwani mwangu mpaka nilipopelekwa hospitali Kanombe kwa matibabu, huenda nikapona lakini mpaka sasa wafanyakazi wetu wangali wananyanyaswa kila kukicha.”

Katika Mkutano ambao uliwakutanisha maafisa wa kilimo na mapori pamoja na uongozi wa wilaya Rubavu,ilidhahirishwa kuwa mnamo mwaka huu 2017 wachungaji waliichungia mifugo yao huchungia maporini na kufanya takriban miti elfu kumi na mbili(12000) na kuharibika na uharibifu huu bado unaendelea.

Na kufuatia hilo waliokuwa wanahudhuria mkutano huo wameomba mikakati madhubuti kuchukuliwa.

Uongozi wilayani Rubavu umesisitiza kuwa hautamsamehe mwenye kukutwa hatia hii ya uharibifu wa misitu, na unyanyasaji wa wanamapori.

Naibu meya anayehusika na mali na maendeleo ya uchumi wilayani, Murenzi Janvier, amesema “kila kukicha miti huwa inauziwa mjini Gisenyi kwenye majengo mapya na inaonekana kuwa mahali pa kupitishwa kuna ngazi za uongozi kwa ujumla, tunamuomba kila mmoja kutekeleza mgogoro huu ili kuwapiga marufuku wahuni hao.

Wameagiza wafugaji wanaochungia mifugo yao kwenye mashamba binafsi kuachana na tabia hiyo na kwamba wachungaji watashauriwa na kuonywa la sivyo hatua za sheria kuchukuliwa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.