kwamamaza 7

RMC yawapa Masharti waandishi wa habari katika wakati huu wa Uchaguzi

0

RMC yaweka masharti ya kuwaongoza waandishi wa habari katika uchaguzi unaokaribia kufanyika katika mwanzo wa Agosti mwaka huu. Ni katika kitabu kilichotangazwa juzi mwa mwisho wa mwezi Juni ambako kunabainishwa orodha ya masharti yaliyoandaliwa na Tume huru ya waandishi wa habari (RCM).

 

Katika Orodha hiyo nzima ya masharti ni pamoja na kutotangaza habari za kuzua ghasia, kuwapa wagombea muda sawa wa kujitetea wakati wa kampeni,matumizi bora ya mitandao na hata kutoegamia upande fulani.

i. Kutotangaza habari za kuzua ghasia

Kwenye sharti la kwamba siyo halali kutangaza habari za kuzua ghasia, waandishi wa habari wanahimizwa kuwa na habari kamili kabla ya kutangaza habari za kutofautiana kwa maneno au matukio mengine yanayazoweza kuleta ghasia.

Kwenye maneno yake kifungo cha sharti hiki kinasema “waandishi wa habari hawanaagizwa kutotangaza madai, ama mgogoro uliozuka kwenye kituo fulani cha uchaguzi bila kuwa na mani ya waliohusika ama kwa upande wa tume ya uchaguzi (NEC).

Wanaoendesha vipindi vya redio na televisheni wanaagizwa kuendesha vipindi hivyo kuhusu uchaguzi kwa kuwahimiza wanaoshiriki vipindi hivyo kutoa maoni ambayo wana uhakika.

ii. Kumwacha mgombea na nafasi ya kujitetea

Vyombo vya habari vinaagizwa kutoacha maoni dhidi ya mgombea kutolewa wakati ambapo mgombea huyo hayuko ili aweze kujitetea. Vyombo vya habari vinahimizwa kufanya kila juhudi kurahisisha watangazaji habari wake kufika mahali kama kwa vituo vya uchaguzi. Na vyombo hivyo vimeagizwa kuwapa mafunzo ya kujinoa kiufundi.

iii. Usalama wa waandishi wa habari

Waandishi wa habari wanahimizwa kujichukulia mikakati ya kujilindia usalama. Ni haki zao kutangaza habari na katika hata mazingira yaliyo hatari kwa usalama wao. Wanaagizwa kuchukuwa vitambulisho vyao ikiwemo kitambulisho, kadi ya waandishi wa habari, na hata cheti cha kutangaza habari kuhusu uchaguzi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wakati ambapo mwandishi wahabari anaonewa ama kuteswa kwa aina yoyote anahimizwa kuripoti mashtaka yake kwenye ngazi za Polisi ya Rwanda, kwa Tume huru ya waandishi wa habari, kwa Tume ya Uchaguzi na hata

iv. Kutopendelea mgombea yeyote

Hii inakuja kusisitiza tabia ya kutobainisha hisia za fulani katika utendaji kazi ya kutangaza habari, waandishi wa habari wanaagizwa kutopendelea chama chochote cha siasa.

Hapa pia kunarudiwa kutofanya kazi tofauti na maadili ya kazi yao.

Kuunganisha stesheni za redio na hata vituo vya televisheni wakati wa vipindi kuhusu uchaguzi nalo limetajwa ni hii ni kwa lengo la kuepukana na upendelevu wa mgombea kwa mwingine.

v. Kutumia ipasavyo mitandao ya kijami

Waandishi wa habri hapa wanaonyeshwa ya kwamba haifai kutangaza maoni yao kwenye mitandao ya kijami bila mpango kwani ingeweza ikaunganishwa na habri za chombo anachokitumikia.

vi. Kuhusu magazeti ya mitandao

Magazeti ya mitandao yanapaswa kuwa na mwongozo wa kuchambua ujumbe wa wasomi wake, wanawajibika kufanya kadri maoni ya wasomi wake hatoaathiri mgombea fulani ikiwa ni kumtusi,kumdhalilisha nakadhalika.

 

 Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

 

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.