kwamamaza 7

Ripoti mpya yahusisha Ufaransa na mauaji ya kimbali nchini Rwanda

0

Ripoti mpya ya serikali ya Rwanda iliyotiwa hadharani leo imeonyesha ushiriki wake katika mipango na utekelezaji katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi.

Ripoti hii ni matokeo ya utafiti wa baraza la wanasheria kwa jina la Cunnigham Levy Muse LLP,Washington,DC.

Ripoti hii inasema kwamba mafisa wa Ufaransa walirahisisha mambo ya kuingiza silaha wakijuwa kwamba kuna mashambulizi dhidi ya Tutsi nchini.

Ripoti hii imeongeza kuwa Wafaransa walijua kuwa kulitokea mauaji ya Tutsi mnamo mwaka 1990 ila walikubali kukutana mjini Kigali na wahalifu wa mauaji ya kimbali na kujadiliana kuhusu uteuzi wa rais wa mpito.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine ni operesheni kwa jina la Turquoise iliyofanya kinyume na misheni yake na kudhamiria kulinda kutondolewa madarakani kwa serikali ya mpito ambayo ilikuwa na hatia ya kutenda mauaji ya kimbali.

Pamoja na haya,taarifa za TNT zinasema kwamba Wafaransa walikana kutoa hati mbalimbali ambazo zingesaidia kutambua vitendo vya Ufaransa nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbali pamoja na kutowatuma watuhumiwa wa mauaji ya kimbali wanaoishi huko.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri wa mambo ya nje,ushirikiano na EAC wa Rwanda,Louise Mushikiwabo amesema kuwa anakubali yaliyomo mwa ripoti hii.

Mala nyingi serikali ya Rwanda huishtaki Ufaransa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994, mashtaka ambayo Ufaransa hukana mno.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.